Skip to content
MASTAA wa kikosi cha Simba ambao wamejiunga na timu hiyo Julai 18 wameanza mazoezi na wachezaji wengine waliotangulia.
Chini ya Kocha Mkuu, Roberto Oliveira kikosi hicho kimeanza maandalizi ikiwa ni kwa ajili ya msimu wa 2023/24.
Ikumbukwe kwamba ni Yanga walitwaa ubingwa msimu wa 2022/23 huku Simba ikigotea nafasi ya pili.
Ni Che Malone Fondoh, Willy Essomba Onana, Aubin Kramo na Jean Baleke wameanza mazoezi ya kurejesha mwili katika ubora.
Wachezaji wengine ambao wameanza mazoezi ni pamoja na nahodha John Bocco, Mohamed Hussein, Shomari Kapombe.