KIPA HUYU WA KAZI KWENYE RADA ZA SIMBA

INAELEZWA kuwa Simba ipo kwenye hesabu za kuinasa saini ya kipa wa kimataifa kuungana na timu hiyo ambayo imeweka kambi Uturuki.

Yanga mlinda mlango namba ni raia wa Mali ambaye anaitwa Djigui Diarra hivyo Simba ikipata saini yake anakwenda kuwa namba mbili.

Namba moja kwa Simba ni mzawa Manula tofauti na Yanga ambapo namba moja ni mgeni Djigui.

Kipa huyo ni raia wa Cameroon Medjo Simon Omossola anayekipiga katika timu ya FC Saint Lupopo ya DR Congo kwa ajili ya kuungana na timu hiyo.

Anatajwa kuja kuchukua nafasi ya kipa namba moja wa klabu hiyo Aishi Manula ambaye ana majeraha ya muda mrefu yanayopelekea kukosekana kwa huduma yake.

Medjo amewahi pia kuhudumu katika timu mbalimbali hapa Afrika zikiwemo Cotton Sport na AS Vital Club.