ONYANGO KUANDALIWA UTAMBULISHO MAALUMU

UONGOZI wa Singida Fountian Gate umeweka wazi kuwa unaandaa utambulisho rasmi kwa nyota wao wote wapya ikiwa ni pamoja na Joash Onyango.

Timu hiyo imeanza maandalizi kuelekea msimu wa 2023/24 na inatarajia kuweka kambi Arusha kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya.

Miongoni mwa wachezaji ambao wamesajiliwa na Singida Fountain Gate ni pamoja na Yahya Mbegu aliyekuwa anacheza Ihefu.

 Ofisa Habari wa Singida Fountain Gate, Hussein Masanza alisema kuwa wameandaa utambulisho maalumu kwa wachezaji wote ambao wamesajiliwa na timu hiyo.

“Tumeandaa utambulisho rasmi kwa ajili ya wachezaji wetu wote ambao wamesajiliwa na wale ambao tunawaongezea mkataba kwa kuwa timu ina utaratibu wake hivyo kila kitu kipo kwenye mpangilio maalumu,”.

Onyango alikuwa Simba ambapo taarifa iliyotolewa na Simba ilieleza kuwa atakuwa Singida Fountain Gate kwa mkopo.