MASHINE NNE ZA SIMBA KUIBUKIA UTURUKI

CLATOUS Chama kiungo wa Simba anatarajiwa kuibukia Uturuki kuungana na wachezaji wenzake baada ya kukamilisha mazungumzo na timu hiyo.

Chama kinara wa pasi za mwisho msimu wa 2022/23 akiwa ametoa 14 alikuwa anatajwa kuwa kwenye hesabu za Yanga.

Hakuwa kwenye msafara wa awali uliokwea pipa kuibukia Uturuki kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2023/24 kutokana na kuwa kwenye mazungumzo na viongozi wa Simba.

Simba waliweka wazi kuwa ikiwa kuna timu itakuwa inamuhitaji Chama iwe ni Yanga, Singida Fountain Gate hawana tatizo muhimu utaratibu ufuatwe.

Ni Jonas Mkude ambaye alikuwa ndani ya Simba msimu wa 222/23 sasa atakuwa ndani ya Yanga 2023/24 baada ya kuibuka Yanga akiwa ni mchezaji huru.

Nyota huyo anatarajiwa kuanza safari Jumatano, Julai 19 akiwa pamoja na nyota mpya Fabrice Ngoma.

Wakati Chama akitarajiwa kuanza safari Jumatano leo mastaa wawili Jean Baleke na Che Malone Fodoh mpango wao wa safari ulitarajiwa kuanza leo.