VIGOGO WA KARIAKOO WAMEDUWAZWA MJINI

UONGOZI wa Dodoma Jiji umeweka wazi kuwa umetibua mipango ya vigogo wa Kariakoo ikiwa ni pamoja na Simba na Yanga zilizokuwa zinaiwinda saini ya Mtenje Albano.

Vigogo hao wameduwazwa kwa kushuhudia saini ya nyota Albano ikiwa ndani ya Dodoma Jiji kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2023/24.

Rasmi ni mchezaji halali wa Dodoma Jiji akitokea ndani ya Coastal Union alikuwa msimu wa 2022/23.

Ofisa Habari wa Dodoma Jiji Moses Mpunga amesema kuwa wameanza kazi baada ya kuwa kimya kwa muda jambo lillikuwa limezua maswali.

“Kulikuwa na maswali mengi kutokana na ukimya wetu tumeanza na Mtenje Albano ambaye alikuwa anawaniwa na timu nyingi ikiwa ni pamoja na vigogo wa Kariakoo lakini sisi tumeshinda na amechagua kuwa mkulima wa Zabibu.

“Wachezaji wengine ambao ni Aboubhakar Ngalema, Collins Opare, Augustino Nsata, Aron Kalambo, David Kibuta hawa watabaki ndani ya Dodoma Jiji yalipo makao makuu na wengine tutaendelea kuwatambulisha,” amesema.

Mbali na Yanga kutajwa kuwania saini ya Albano hata Namungo FC ilikuwa inatajwa kuwa kwenye hesabu za kuiwania saini ya mzawa huyo.