UZI WA SIMBA KUZINDULIWA KILELENI, KILIMANJARO

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa uzi mpya wa msimu wa 2023/24 upo tayari na utazinduliwa Kilimanjaro.

Kikosi cha Simba kimeweka kambi Uturuki na kwa sasa maandalizi kuelekea msimu mpya yanaendelea ikiwa ni pamoja na suala jezi mpya.

Ipo wazi kuwa watani zao wa jadi Yanga wao uzi upo mtaani baada ya uzinduzi wao kukamilika.

Yanga wao walizindua uzi Malawi na baada ya uzinduzi uzi wa Yanga ulikuwa unapatikana kila kona na rangi nyeusi inatajwa kuwa pendwa na mashabiki.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Iman Kajuna amesema:”Nawambia rasmi hapa kwamba jezi ya Simba itazinduliwa juu ya Mlima Kilimanjaro ikiwa ni historia na mipango ipo tayari na kila kitu kinakwenda sawa.

“Jezi itaanza kupandishwa mlimani siku ya Jumatano na watakuwa kileleni siku ya Ijumaa na Jumamosi jezi itakuwa kwenye maduka yote nchini,” .

Wakati huohuo Simba Day itakuwa ni Agosti 6 badala ya Agosti 8 kwa kuwa Agosti 10 watakuwa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Singida Fountain Gate, Mkwakwani, Tanga.