HILI HAPA JEMBE JIPYA YANGA

MIAKA miwili kasaini mwamba Yao Kouas Attouhula akitokea Klabu ya ASEC Mimosa kuwa ndani ya Klabu ya Yanga.

Ikumbukwe kwamba timu hiyo aliwahi kucheza Aziz Ki ambaye ni kiungo wa Yanga anayevaa jezi namba 10.

Huyu anakuwa nyota watano kusajiliwa ndani ya Yanga baada ya Nickson Kibabage, Gift Fred,Jonas Mkude na Maxi Mpia

Yeye ni beki anaweza kucheza kulia na kushoto akiwa uwanjani hivyo anakuja kuongeza nguvu kwenye eneo la ulinzi ndani ya Yanga.

Yanga imeweka wazi kuwa huyo ni mchezaji mkubwa ambaye amechagua timu kubwa na ya makombe.

Ikumbukwe kwamba Yanga imetwaa Ngao ya Jamii, ligi, Kombe la Azam Sports Federation ikiwa imeweka kambi Kigamboni kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2023/34..