MAJEMBE MENGINE YANASHUSHWA YANGA

MAXI Mpia Nzengeli ni ingizo jipya ndani ya Yanga akitokea kikosi cha Maniema ya Dr Congo.

Yeye ni winga mwenye uwezo wa kupandisha mashambulizi na kufunga jambo ambalo limewavutia Yanga kuinasa saini yake.

Nyota huyo mpya Yanga anaungana na wengine ambao wametambulishwa ndani ya Yanga ikiwa ni mzawa Nickson Kibabage aliyekuwa wa kwanza kutambulishwa.

Mwingine ni kiungo Jonas Mkude aliyekuwa anakipiga ndani ya Simba tangu 2010 na sasa anapata changamoto mpya ndani ya Yanga.

Pia Gift Fred huyu ameanza mazoezi na wachezaji wenzake wa Yanga baada ya kutambulishwa.

Yanga inatarajiwa kuendelea kushusha mashine nyingine za kazi kwa ajili ya kusuka upya kikosi hicho ambacho tayari kimeanza mazoezi Avic Town na Julai 22 inatarajiwa kuwa Wiki ya Mwananchi ambapo watacheza na Kaizer Chiefs mchezo wa kirafiki.

.