KWENYE usajili wa Simba katika dirisha lililofunguliwa hivi karibuni ni mzawa mmoja ametambulishwa ambaye ni David Kameta, ‘Duchu’.
Moja ya mabeki wenye juhudi kwenye timu za kati amerejea ndani ya kikosi cha Simba anajukumu la kupambana kufikia uwezo wa kufanya kweli.
Wapo wazawa wengi ambao waliibuka ndani ya Simba kutoka timu za madaraja ya kati wakashindwa kuonyesha makeke yao.
Sio wazawa tu wapo hata wageni amao wamekwama kuonyesha thamani ya nembo ya Simba mfano Peter Banda bado anajitafuta kujenga kibanda ndani ya Simba.
Pia kwenye upande wa mlinda mlango bado Ally Salim anapaswa kuwa na changamoto nyingine kwa kuwa Aishi Manula hajawa fiti kwa asilimia 100.
Tetesi zinaeleza kuwa Simba imemalizana na kipa kutoka nje ya nchi ambaye atakuwa kikosini nchini Uturuki, yote kheri ikiwa wanahitaji kufanya vizuri lazima wawe imara kila idara.
Niliwahi kusema kuwa Simba kumuacha Beno Kakolanya kwa nyakati hizi ilikuwa ni moja ya mtihani kwao lakini wao wanapanga na wanajua ambacho wanakifanya.
Kakolanya ni moja ya makipa bora kwa wazawa akipata timu atafanya vizuri na inaelezwa anaweza kuibukia Singida Fountain Gate.