HAMISI Kassimu Ndigo mkazi wa Kijichi ambaye ni muuza Chipsi Dar ni mshindi wa bonasi ya Super Jacpot ya SportPesa baada ya kupatia kwa usahihi mechi 15 kati ya 17 na kushinda Tsh. 5,908,578.
Mshindi huyo wa SportPesa Hamisi amesema kuwa alianza kucheza na SportPesa miaka mitatu iliyopita kutokana na marafiki zake kucheza na kushinda vitita vya multibet na Jackpot SportPesa.
“Mimi nilianza kucheza na SportPesa 2020 wakati ule nikiwa bado maeneo ya Mtoni Kijichi. Nilikuwa nawaona washikaji zangu wanacheza na kushinda na SportPesa.
“Mimi nikawaomba wanifundishe na walikubali na kunifundisha. Nilianza mdogomdogo nikicheza timu mbili tatu hadi nilipoweza kucheza kuanzia timu nane mpaka timu kumi.
“Kwa bahati nzuri toka nimeanza na kujua kucheza nilibahatika kushinda Tsh 18,000 mara moja katika multibet. Ushindi huu ulinipa moyo sana na kunifanya kuendelea kucheza hata kama baadae sikushinda chochote.
“Sikuruhusu kukata tamaa, kwani niliamini kama watu wengine walikuwa wanashinda basi na mimi ninanafasi sawa na wao ya kushinda hivyo niliendelea. Safari hii nilianza kucheza zaidi Jackpot za SportPesa.
“Unajua katika kucheza michezo hii kuna maneno mengi. Mengine ya kutia moyo na mengine ya kukatisha tamaa. Unaweza kukutana na watu na wakijua unabashiri, basi wataanza kukwambia maneno ambayo yatakukatisha tamaa. Mimi sikukata tamaa niliendelea kucheza na matokeo yake ndio haya nimeshinda Supa Jackpot bonus.
“Kila mwanzo wa wiki huwa naangalia mechi za Jackpot kupitia simu yangu janja, ila wakati wa kucheza nacheza kwa kutumia simu ya tochi au kiswaswadu.
‘’Mimi huwa na kawaida kila Jumatatu na Ijumaa kuingia mtandaoni na kutizama kama mechi za Jackpot zimetoka au la. Ikiwa zimetoka basi hujitahidi ifikapo usiku wakati nimemaliza shughuli zangu, napitia mechi moja moja kisha naweka mkeka wangu wa Jackpot.
“Sikuwa na muda wa kufuatilia sana matokeo kutokana na ubize katika eneo langu la kazi, kwa kuwa kulikuwa na wateja wengi siku hiyo ya Jumamosi. Kuna sms iliingia mida ya saa saba kama na dakika 20 za usiku.
“Baada ya kumaliza kazi za usafi nikiwa nafunga kazi niliamua kutizama simu na kukutana na habari njema ya ushindi kupitia sms kutoka SportPesa.
“Kwa muda ule nilifurahi sana na kuduwaa kidogo. Si unajua pesa hii kwa sisi wa uswahilini ni nyingi kidogo. Nilijaribu kutoa pesa nikashindwa hivyo nililala mpaka asubuhi na kuwasiliana na watoa huduma kwa wateja wa SportPesa ambao walinielekeza nahitaji kuja ofisi za SportPesa kwa ajili ya uhakiki na kukabidhiwa mfano wa hundi.
“Nashukuru mtoa huduma kwa wateja alinielekeza vizuri, hivyo kupelekea mimi kuja hapa ofisi za SportPesa kwa ajili ya uhakiki na taratibu za ki utawala.
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa kampuni ya SportPesa Sabrina Msuya amempa pongezi mshindi huyo na kumwambia kwamba aendelee kucheza.
‘’Nampa pongezi Hamisi kwa kufanikiwa kushinda bonasi ya Supa Jackpot, vile vile nitoe rai kwake aendelee kucheza hizi Jackpot bila kukosa kwani kila mchezaji ana nafasi sawa katika kushinda zawadi zetu, iwe kiwango kikubwa au kiwango cha kawaida.
“Mwisho ni kuwakumbusha watanzania kuendelea kucheza na SportPesa kwani mkwanja upo wa kutosha na bidhaa za kukupa mikwanja zipo. Unaweza cheza Jackpot zote mbili, unaweza cheza michezo ya Kasino kama Aviator na Virtual Football Pro au multibet ambayo ina bonasi ya mpaka asilimia 1000 ya ushindi ambao utaupata,”.
Safari hii mkwanja bado upo na Supa Jackpot ya SportPesa wiki hii imesimamia TZS 1,131,423,064.