YANGA KAZI IMEANZA, MAJEMBE YANANOLEWA

KIKOSI cha Yanga kimeanza mazoezi ikiwa ni maandalizi ya msimu wa 2023/24.

Timu hiyo ya Yanga imeweka kambi Avic Town Kigamboni ikiwa chini ya Kocha Mkuu Miguel Gamondi.

Miongoni mwa mastaa wa Yanga ambao wameanza mazoezi ni pamoja na ingizo jipya Gift Fred, Kennedy Musonda, Aboutwalib Mshery na Dickson Job.

Majembe hayo yananolewa ikiwa ni kuwa tayari kwa ajili ya msimu mpya ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Yanga ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara baada ya kutwaa msimu huu huku watani zao wajadi Simba wakigotea nafasi ya pili.