YANGA YATAMBULISHA JEMBE JIPYA

RASMI Julai 11 2023 Yanga imemtambulisha nyota mpya Gift Fred kutoka SC Villa ya Uganda kuwa mali yao.

Nyota huyo tayari aliwaaga mashabiki na viongozi wa timu yake ya zamani kwa kuwaambia Thank You hivyo anakuja Bongo kwenye changamoto mpya.

Yote haya ni maboresho ndani ya Yanga kwa ajili ya msimu mpya wa 2023/24 na kami yao itakuwa ni Kigamboni.

Ni Nikson Kibabage huyu ni mchezaji wa kwanza kutambulishwa ndani ya kikosi cha Yanga na wengine wanafuata.

Mwamba huyu ni beki ambaye dili lake likikamilika atakuja kuongeza nguvu kwenye eneo la ulinzi.