Skip to content
KUTOKA Mtibwa Sugar inayotumia Uwanja wa Manungu kwa mechi za nyumbani amerejea ndani ya kikosi cha Simba beki wa kupanda na kushuka.
Beki huyo ni shuhuda Yanga wakitwaa ubingwa wa ligi msimu wa 2022/23 huku Simba ikigotea nafasi ya pili.
Mchezo wa kwanza kwa Simba utakuwa wa Ngao ya Jamii dhidi ya Singida Fountain Gate unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Ni Geita Gold aliaza kisha akaibukia Mtibwa Sugar na sasa ni ndani ya Wekundu wa Msimbazi.
Anaitwa David Kameta wengi wanapenda kumuita Duchu beki wa kulia.
Julai 10 usiku saa tatu alitambulishwa ndani ya kikosi cha Simba akiwa ni mzawa wa kwanza kutambulishwa ndani ya kikosi hicho.
Wazawa wawili wameongezewa mikataba yao ambao ni Shomari Kapombe na Mohamed Hussein.
Wote hawa ni mabeki ikiwa ni maandalizi ya kuelekea msimu mpya wa 2023/24 ambapo Simba wanatarajia uweka kambi Uturuki.