NI Che Malone Fondoh yeye ni beki ametambulishwa ndani ya kikosi cha Simba ikiwa ni ingizo jipya kwa washindi hao wa pili kwenye ligi.
Yanga ni mabingwa wakiwa ni washindi wa kwanza ambapo nao wanajipanga kwa ajili ya kupambania ubingwa wao.
Timu hizo za Yanga na Simba ikiwa kila timu itashinda kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali ya Ngao ya Jamii huenda wakakutana kwenye hatua ya fainali, Mkwakwani, Tanga.
Nyota ambaye ametambulishwa leo Julai 9,2023 ni raia wa Cameroon mwenye miaka 24 amesaini dili la miaka miwili.
MVP wa Ligi Kuu ya Cameroon 2022/23 alitwa timu ya taifa ya Cameroon kuwania kufuzu AFCON pamoja na kikosi cha wache