MATAJIRI wa Dar, Azam FC msimu mpya wa 2023/24 watafungua kete yao ya kwanza kwa kucheza na Yanga katia mchezo wa Ngao ya Jamii.
Azam FC wataanza msimu mpya wa 2023/24 kwa kucheza mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga, utakaofanyika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga Agosti 2023.
Mchezo huo utachezwa saa 1.00 usiku kwa kuwa miundombinu ya Tanga inaruhusu kuchezwa mechi usiku baada ya ukarabati.
Mshindi wa mchezo huo, atakutana kwenye fainali na mshindi wa nusu fainali nyingine itakayowakutanisha Simba SC na Singida Fountain Gate FC.
Michuano hiyo ya Ngao ya Jamii, itahimishwa Agosti 13 kwa mchezo wa fainali pamoja na mechi nyingine ya kutafuta mshindi wa tatu.
Tayari Azam FC imeanza maandalizi kuelekea msimu mpya ikiwa na nyota kama Sopu, Fei Toto, Dube na Idris Mbombo.