JOASH Onyango beki wa Simba rasmi kwa msimu wa 2023/24 atakuwa kwenye changamoto mpya na timu mpya ndani ya Singida.
Nyota huyo mkataba wake na Simba unatarajiwa kumeguka msimu ujao na mabosi wa Simba wamefikia makubaliano ya kumtoa kwa mkopo kuelekea Singida Fountain Gate.
Atakuwa ndani ya Singida Fountain Gate kwa mkopo msimu wa 2023/24 kwenye changamoto mpya.
Ikumbukwe kwamba Julai 7 ilivuja picha ikimuonyesha Onyango akiwa na uzi wa Singida Fountain Gate FC na leo Julai 8 Simba wametaoa taarifa rasmi kuhusu mchezaji wao.