BEKI WA KAZI SIMBA ATAJWA KUIBUKIA SINGIDA

BEKI wa kazi ndani ya kikosi cha Simba Joash Onyango anatajwa kuingia kwenye rada za Singida Fountain Gate yenye maskani yake Singida.

Jioni ya Julai 8 2023 ilikuwa ikisambaa picha iliyokuwa inamuonyesha mtu aliyefanana na Onyango akiwa ameshika mkataba wa Singida Fountain Gate.

Taarifa zinaeleza kuwa picha hiyo imevujisha na mmoja ya watu wanaohusika na usajili huku wengine wakieleza kuwa sio picha halisi bali ni ile ya kutengenezwa.

Ofisa Habari wa Singida Fountain Gate, Hussein Masanza aliweka wazi kuwa taarifa zote za usajili zikiwa tayari zitatolewa.

“Kila kitu kina utaratibu wake na taarifa za usajili zikikamilika zote zitatolewa kwa wakati kwenye vyanzo vyetu sahihi,”.