SIMBA YATANGAZA KOCHA MPYA

RASMI Simba imetangaza kocha mpya wa makipa kwa ajili ya kuwa na timu hiyo kwa msimu wa 2023/24.

Ikumbukwe kwamba kocha huyo alikuwa ni shuhuda wa Yanga wakitwaa ubingwa wa ligi msimu wa 2022/23 alipokuwa ndani ya Azam FC.

Pia alishuhudia Azam FC ikipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Yanga kwenye mchezo wa fainali wa Azam Sports Federation, Tanga ukiwa ni mchezo wake wa mwisho kuwa na uzi wa Azam FC.

Ni Daniel Cadena ambaye alikuwa akiwafundisha makocha wa Azam FC sasa atakuwa ndani ya kikosi cha Simba.

Julai 6 ametangazwa kocha huyo kuungana na timu hiyo ambayo inatarajia kuweka kambi Uturuki kwa maandalizi ya msimu mpya.

Cadena ameweka wazi kuwa ni furaha kwake kuwa na timu hiyo anaamini atafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa.