NYOTA WA YANGA WATAMBULISHWA GROUP LA WhatsApp

IMEFAHAMIKA kuwa Singida Fountain Gate tayari imefanikiwa kuwasajili nyota wawili kutoka Yanga, David Bryson na Dickson Ambundo ambao tayari wametambulishwa kwa wachezaji wenzao kupitia Group la WhatsApp.

Tayari Ambundo amekutana na ‘Thank You’ Yanga baada ya kutangaza kuachana nao katika msimu ujao kutokana na mkataba wake kumalizika.

Chanzo cha habari kutoka kwa mmoja wa viongozi wa Benchi la Ufundi la Singida Fountain Gate kilieleza kuwa usajili wa wachezaji hao wote umekamilika na wanachosubiriwa ni kutambulishwa kupitia kurasa za mitandao ya kijamii inayoendeshwa na timu hiyo.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa viongozi wa benchi la ufundi na wachezaji tayari wametambulishwa nyota hao baada ya kuungwa katika Group la WhatsApp la timu kwa ajili ya kupata taarifa za maandalizi.

Singida Fountain Gate tunaendelea kuzidi kujiimarisha baada ya kukamilisha usajili wa wachezaji wetu wawili kutoka Yanga, beki wa kushoto Bryson na kiungo mshambuliaji Ambundo.

“Ambundo yeye alitangazwa kuachana na Yanga wiki iliyopita baada ya kumaliza mkataba na timu hiyo. Upande wa Bryson yeye hadi jana Jumanne alikuwa bado hajatangazwa lakini yupo tayari mkoani Singida.

“Wachezaji hao tayari wameshasajiliwa na wapo kwenye kundi la timu hiyo la WhatsApp kwa ajili ya kupata taarifa zote za timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao,” kilisema chanzo hicho.

Alipotafutwa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Hans Pluijm kuzungumzia hilo alisema kuwa: “Mimi kocha kazi yangu ni kupendekeza usajili pekee, na uongozi kukamilisha hivyo hilo niwaachie hao.”