NYASA BIG BULLETS YATOSHANA NGUVU NA YANGA

KWENYE mchezo maalumu wa kutimiza miaka 59 ya Uhuru wa Malawi timu zote mbili zimetoshana nguvu kwa kutofungana.

Ubao umesoma Nyasa Big Bullets 0-0 Yanga ambapo Yanga walitumia asilimia kubwa wachezaji wa timu ya vijana.

Kwenye mchezo wa leo kiungo Dennis Nkane alipata maumivu yalipolekea ashindwe kuendelea na mchezo huo lakini hali yake kwa sasa inaendelea vizuri baada ya kupata matibabu.

Kipa namba mbili wa Yanga, Metacha Mnata alionyesha umakini wake katika kutimiza majukumu yake uwanjani.

Hatari tatu za kipindi cha pili ziliokolewa na kipa huyo kutoka kwa washambuliaji wa Big Bullets ambao walikuwa wanahitaji kumfunga mwamba huyo.