MAJEMBE MAWILI YA KAZI NDANI YA AZAM FC

MASTAA wawili wametambulishwa ndani ya Azam FC kwa ajili ya msimu wa 2023/24 unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Tayari 2022/23 imegota mwisho huku mabingwa wakiwa ni Yanga waliotwaa taji hilo chini ya Nasreddine Nabi.

Yanga kwa sasa inaendelea na maboresho ya timu kupambana na wapinzani wao msimu ujao ikiwa ni pamoja na Azam FC ambao wamekuwa wakileta ushindani mkubwa kwenye ligi.

Ni Alassane Diao ambaye ni mshambuliaji huyu anatokea US Green bonge moja ya jitu limekwenda hewani.

Nyota huyu ni mshambuliaji raia wa Senegal kasaini kandarasi ya miaka miwili alitambulishwa rasmi Julai 4, 2023.

Mwingine ni Cheikh Tidiane Sidibe huyu ametoka Teungueth ana miaka 24 ni beki wa kushoto na mtaalamu wa mapigo huru.

Anatokea Senegal ni dili la miaka miwili kapewa kuitumikia timu hiyo inayotumia Uwanja wa Azam Complex.