BREAKING:ONANA NI MALI YA SIMBA

NI Essomba Onana nyota mpya ndani ya kikosi cha Simba ukiwa ni usajili wa kwanza kutangazwa kuelekea msimu wa 2023/24.

Nyota huyo amepewa dili la miaka miwili alikuwa anakipiga ndani ya Rayon Sports.

Mwamba huyo anakuja kushiriki ligi ya Bongo akitokea Rwanda huku mabingwa watetezi wakiwa ni Yanga.

Simba inatarajiwa kuweka kambi Uturuki kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya ipo chini ya Kocha Mkuu, Roberto Oliveira.

Msimu wa 2022/23 imegotea nafasi ya pili ambapo imeachana na baadhi ya wachezaji ikiwa ni pamoja na Jonas Mkude, Erasto Nyoni ambaye ametambulishwa ndani ya Namungo.