MTIBWA SUGAR WAJENGA NGOME YAO

MTIBWA Sugar U 20 ni mabingwa mara ya tano katika Ligi ya Vijana ukiwa ni utawala mkubwa kwao.

Sio Azam FC, Simba, Yanga wala Geita Gold ambao wamefanikiwa kuonyesha makeke mbele ya timu hiyo.

Katika fainali iliyochezwa Julai 2, 2023 Uwanja wa Azam Complex waliibuka washinda kwenye mchezo huo.

Ubao wa Uwanja wa Azam Complex ulisoma Mtibwa Sugar 1-0 Geita Gold na mtupiaji akiwa ni Makambo dakika ya 97.

Washindi wa tatu ni Azam FC ambao waliibua na ushindi wa mabao 3-1 Kagera Sugar huku Cyprian Kachwele akifunga mabao yote matatu.