KIVUMBI NA JASHO LEO FAINALI U 20

KIVUMBI kinatarajiwa kutimka leo Julai 2 kwa mchezo wa fainali ya Ligi ya Vijana U 20 kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya Geita Gold.

Mtibwa Sugar walifanikiwa kuingia fainali baada ya ubao wa Uwanja wa Azam Complex kusoma Mtibwa Sugar 2-1 Azam FC huku Geita Gold wao ubao ulisoma Kagera Sugar 0-2 Geita Gold.

Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Awadh Juma amesema kuwa wanatambua kwamba kazi itakuwa kubwa ila watapambana kupata matokeo mazuri.

“Fainali ni fainali tunajua utakuwa mchezo mzuri na tupo tayari kwa ajili ya mchezo huo hivyo mashabiki wajitokeze,” .

Choke Abeid, kocha wa Geita Gold U 20 alisema kuwa wanatambua fainali itakuwa ngumu hivyo wanajipanga kupata matokeo.

“Fainali ni fainali tunawaheshimu wapinzani wetu na tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu ambao utakuwa na ushindani mkubwa,”.

Fainali hiyo itapigwa baada ya kushuhudia mchezo wa kumsaka mshindi wa tatu kati ya Azam FC dhidi ya Kagera Sugar itakayopigwa saa 9:00 alasiri.

Burudani zote hizi zinatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex ambapo bingwa atafahamika baada ya dakika 90 za mchezo.

Yanga na Simba U 20 wote watakuwa mashuhuda wa bingwa mpya leo kwa kuwa hakuna timu iliyofanya vizuri kwenye mashindano hayo.