YANGA IMETENGENEZA MKWANJA MREFU, MIPANGO KAZI

Rais wa Yanga Eng. Hersi Said ameweka wazi kuwa Yanga imetengeneza zaidi ya bilioni 7 kutokana na wadhamini mbalimbali pamoja na kuiheshimisha Tanzania kimataifa.

Ni Juni 24 kwenye mkutano wa Wanachama wa Yanga aliweka wazi hayo kuhusu mafanikio ambayo wamefikia pamoja na muonekano wa uwanja mpya wa Yanga utakavyokuwa.

Hiyo ni kwa msimu wa 2022/23 Klabu ya Yanga imefanikiwa kutengeneza zaidi ya Tsh. 7 bilioni. Fedha hizo zinatokana na wadhamini mbalimbali wa klabu hiyo.

Amesema pia Yanga imeingiza zaidi ya Tsh. 3 bilioni kupitia mafanikio yaliyotokana na ushiriki wa mashindano mbalimbali na mapato yanayotokana na viingilio vya mechi.

Aliongeza kuwa baada ya kupewa dhamana ya kuiendesha klabu Yanga kupitia Mkutano Mkuu uliopita, waliweka mpango kazi na kuwahakikishia mambo matano.

“Tukio la kwanza kubwa lilikuwa ni Wiki ya Mwananchi.Tuliweka historia ambayo haijawahi kufikiwa nchini kwa kuingiza mapato ya zaidi ya Tsh. 520 kwenye mechi moja ya Wiki ya Mwananchi.

“Kuhakikisha kwamba tunaleta mataji, watu walikuwa wanataka kuona tutafanya nini uwanjani.Tulifanikiwa kuchukua Ngao ya Jamii mwaka 2022. Tumechukua ubingwa wa NBC Premier League 2022/23 na kuweka historia ya kufikisha unbeaten 49 kwa mara ya kwanza kwenye historia nchini lakini unbeaten ya nne Afrika.

” Tumechukua Kombe la mashindano ya Azam Sports Federation 2022/23.Baada ya msimu uliopita kuweka jitihada kwenye mashindano ya ndani, msimu huu tukasema ni msimu wetu kwenye mashindano ya kimataifa. Kwa mara ya kwanza katika nchi hii medali ya kwanza ya CAF Confederation Cup imetua Tanzania kupitia Yanga.

“Tumefanikiwa kuiheshimisha Yanga na Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa na bado mipango inaendelea kwa ajili ya kufanya vizuri zaidi,” amesema.