MASTAA wanne wameachwa mazima ndani ya kikosi cha Yanga kuelekea kwenye mpango kazi wa kuunda kikosi kipya kwa msimu wa 2023/24.
Juni 23 beki Abdallah Shaibu, ‘Ninja’ anafikisha idadi ya nyota wanne ambao hawatakuwa kwenye kikosi hicho kilichotwaa ubingwa wa ligi msimu wa 2022/23.
Taarifa rasmi kutoka Yanga imeeleza kuwa: “Tunamshukuru Abdallah Shaibu (Ninja) kwa mchango wake katika kipindi chote alichokuwa nasi na tunamtakia kila la kheri katika maisha yake mapya nje ya Young Africans SC,”.
Wengine ambao watakuwa nje ya Yanga ni pamoja na kiungo Bernard Morrison raia wa Ghana alitupia mabao matano kibindoni mbali na kufunga alitoa pia pasi pasi mbili za mabao.
Dickson Ambundo winga mzawa aliyeibuka ndani ya Yanga akitokea Dodoma Jiji pamoja na mzee wa spidi 120 Tuisila Kisinda raia wa DR Congo.