LICHA ya mashabiki wa Mbeya City kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Sokoine mambo yamekuwa magumu kwa timu hiyo kusalia ndani ya Ligi Kuu Bara.
Baada ya dakika 90 ubao umesoma Mbeya City 0-1 Mashujaa kutoka Kigoma wakipeta kwa ushindi wa jumla ya mabao 1-4.
Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Kigoma ubao ulisoma Mashujaa 3-1 Mbeya City hivyo Mbeya City walikuwa wanapambana kusaka ushindi huku Mashujaa wakipambana kulinda ushindi wao.
Bao la mashujaa limepachikwa dakika ya 87 liliwavuruga Mbeya City huku mmoja wa kiongozi kutoka Mashujaa katika harakati za kushangilia alionekana akimpiga kocha wa Mbeya City jambo lililopelekea kuonyeshwa kadi nyekundu.
Rasmi Mbeya City inaungana na Ruvu Shooting, Polisi Tanzania kuwa timu ambazo zitashiriki Championiship msimu wa 2023/24