BREAKING:KOCHA MPYA YANGA HUYU HAPA

RASMI Miguel Angel Gamondi raia wa Argentina ametangazwa kuwa kocha mpya wa Yanga.

Kocha huyo anachukua mikoba ya Nasreddine Nabi ambaye amefikia makubaliano ya kutongeza mkataba na timu hiyo.

Nabi kwa misimu miwili aliyokuwa na kikosi cha Yanga ameiongoza kutwaa mataji mawili ya ligi mfululizo pamoja na kutinga hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Kocha huyo ameweka wazi kuwa ana uzoefu na soka la Afrika jambo ambalo halimpi tabu kwenye maisha mapya ndani ya Yanga.

“Ninatambua soka la Afrika nina amini kwamba tutafanya vizuri kwa ushirikiano wa wachezaji pamoja na viongozi,”.