KUTOKA Dodoma mpaka Dar kutokana na uwezo wake ambao uliwavutia mabosi wa Yanga wakampa dili kuitumikia timu hiyo.
Alikuwa anacheza ndani ya Dodoma Jiji akaanza changamoto mpya Yanga yenye maskani yake Jangwani, Kariakoo.
Mafanikio makubwa akiwa na timu hiyo ni pamoja na kuwa miongoni mwa wachezaji walioandika historia ya kutinga hatua ya fainali katika Kombe la Shirikisho Afrika ni rekodi yake kubwa kuliko akiwa na Yanga.
Anaitwa Dickson Ambundo winga mwenye uwezo mkubwa wa kutumia mguu wa kulia katika kufanya kazi yake aipendayo ya mpira.