Skip to content
KUELEKEA msimu wa 2023/24 mabosi wa Azam FC wamemuongezea dili la miaka mitatu nyota Sospeter Bajana.
Nyota huyo bado ataendelea kusalia ndani ya Azam FC inayotumia Uwanja wa Azam Complex mpaka 2026.
Ikumbukwe kwamba Azam FC iligotea nafasi ya pili kwenye fainali ya Azam Sports Federation baada ya kupoteza kwenye mchezo dhidi ya Yanga.
Yanga pia ni mabingwa wa ligi wakikamilisha msimu nafasi ya kwanza na pointi 78.
Timu hiyo imemaliza msimu wa 2022/23 ikiwa nafasi ya tatu chini ya Kali Ongala ambaye amepewa mkono wa asante.
Bajana anakuwa mchezaji wa kwanza kupewa dili la kuongeza mkataba ndani ya Juni 2023 kwa ajili ya msimu mpya.
Ni Feisal Salum huyu ni mchezaji wa kwanza kutambulishwa ndani ya Azam FC kwa kusaini dili la miaka mitatu akitokea Yanga.