HESABU ZA KESHO MUHIMU KUPANGWA LEO

KWA kila aina ya nyakati ambazo zinapita ni muhimu kuwa na mwendelezo mzuri ambao utaleta matokeo chanya kila idara kwenye sekta ya michezo sio Yanga tu bali Singida Big Stars.

Namungo mpaka Geita Gold wakati wa kuanza maandalizi ni sasa kwani kila timu ni muhimu kufanya maandalizi mazuri.

Wapo ambao wanaamini kwamba kufika mwisho kwa ligi kazi imeisha hivyo msimu ujao mambo yatakuwa kama ilivyo kwa sasa.

Tunaona timu zimewapa wachezaji likizo ikiwa ni kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya huku dirisha la usajili likitazamwa kuwa kipindi cha kazi.

Licha ya kwamba ni muda wa mapumziko ni muhimu kwa wachezaji kutambua kwamba lazima wapambane kujiweka tayari kwa ajili ya msimu ujao.

Wanasema liishalo ni dogo kuliko lile linalokuja hivyo msimu ujao utakuwa na ushindani mkubwa kuliko hata huu ambao tayari umepita.

Kila timu itakuwa kwenye mpango kazi wa kupata matokeo chanya na haitakuwa rahisi ikiwa hakuna ambaye atakuwa amejipanga vizuri.

Maandalizi ni muhimu kwa timu kupata matokeo mazuri na kupata muda wa kupumzika kwa wakati muda huu wa likizo.

Tunatarajia kuona muda wa likizo unatumika vizuri na kila idara kwa kutafuta sehemu nzuri kwa ajili ya kambi pamoja na eneo zuri la kutuliza akili.

Baada ya kupambana kwa muda na ligi kugota mwisho ni muda wa kuwa pamoja na familia pamoja na kuongeza nguvu kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.

Kila kitu kinawezekana kuwa bora ikiwa utaamua kiwe bora na kitakuwa hafifu ikiwa utaamua kiwe hafifu huu ni muda wa kupanga hesabu za kesho.