DJUMA Shaban na Yannic Bangala wanatajwa kuomba kuondoka ndani ya kikosi cha Yanga.
Habari zinaeleza kuwa kuondoka kwa Nasreddine Nabi ndani ya Yanga kwenye benchi la ufundi kunawafanya mastaa wengine kufikiria kuondoka pia.
Ipo wazi kuwa Bangala mkataba wake bado unaishi ndani ya Yanga kama ilivyo kwa Djuma mpaka 2024 lakini wanahitaji kuondoka.
Djuma ameomba kuondoka Yanga ili kupata changamoto mpya na Bangala pia ameomba kusepa licha ya kuwa na mkataba wa mwaka mmoja.