>

WAZAWA KUPWA NA KUJAA KUFIKE MWISHO

WAZAWA ipo wazi kuwa hawajawa na msimu mzuri kutokana na rekodi kuwakataa ndani ya uwanja kwenye kila idara.

Ni Yanga kinara wa utupiaji ni Fiston Mayele raia wa DR Congo ni Clatous Chama wa Simba kinara wa pasi za mwisho.

Mayele ametupia mabao 16 ndani ya kikosi cha Yanga na Chama pasi 14 sio hawa tu hata Singida Big Stars kinara wa mabao ni Brnuo Gomes raia wa Brazil katupia mabao 10.

Meddie Kagere naye yupo ndani ya Singida Big Stars katupia mabao 9 huku ndani ya Dodoma Jiji ni Collins Opare katupia mabao 9 yeye ni raia wa Ghana.

Angalau kipindi fulani ilikuwa upande wa mlinda mlango kwa namna yoyote ile atakuwa mzawa kafanya vizuri lakini mambo yamebadilika na kila siku afadhali ya jana.

Wageni wamekuwa wafalme kwenye kila idara kuanzia eneo la ushamuliaji, viungo mpaka kwenye lango hii ni somo ambalo linapaswa kuchukuliwa kwa uzito.

Wapo wazawa wenye uwezo lakini jitihada zao wamekuwa wakizificha na kuonyesha kwenye baadhi ya mechi kisha mechi nyingine kushindwa kuendeleza makali yao.

Uwezo wa wazawa umekuwa ni maji kupwa maji kujaa leo anafanya kazi kwa ustadi kisha kesho anakuja na mbinu nyingine ambazo hata muda mwingine benchi la ufundi linakwama kuelewa sababu ya kuwa kwenye mwendo huo.

Ya msimu wa 2022/23 yanakwenda kufungwa ambapo ukurasa mpya unatarajiwa kwenda kufunguliwa wakati ujao .

Hapo ni wakati wa kutumia makosa ambayo yametokea kwenye mzunguko huu na kufanyia kazi kwa umakini kupata matokeo mazuri.

Ushindani mzuri ni ule kila mmoja anafanya kazi kubwa na nzuri kwenye kila idara pale mmoja anapotawala kila idara hii sio picha nzuri.

Haina maana kwamba wazawa hawafanyi kazi nzuri hapana hapa tunazungumzia mwendo bora kila wakati kuna mahali wanakwama kuwa na kile kitu ambacho wanakupa kwenye mchezo mmoja.

Ubora wa wachezaji wazawa umekuwa ni wa tofauti kwenye kila mchezo kulingana na mahitaji ya benchi la ufundi ni muda wa kufanyia kazi makosa na kurejea imara wakati ujao.

Nahodha John Bocco alianza kwa kasi msimu wa 2022/23 akitupia mabao 9na hat trick mbili ambazo amegotea nazo hapo mpaka sasa.