SIMBA YAICHAPA COASTAL UNION, SAIDO ATUPIA

KIKOSI cha Simba kimeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Coastal Union uliochezwa Uwanja wa Uhuru huku kikigotea nafasi ya pili vinara ni Yanga.

Yanga ni namba moja kwenye msimamo wakiwa wamepata ushindi mbele ya Tanzania Prisons, Mbeya.

Simba imekamilisha kazi yake kwa msimu wa 2022/23 ikiwa ni kupitia kwa Saido Ntibanzokiza aliyepachika mabao mawili dakika ya 13 na 73.

Bao la pili kwa Simba lilifungwa na John Bocco dakika ya 56 ikiwa ni bao lake la 10 kwenye msimu,

Bao pekee la Coastal Union limepachikwa na Amza Moubarack dakika ya 7 kwa mkwaju wa penalti.

Ntibanzokiza anafikisha jumla ya mabao 17 kwenye ligi sawa na nyota wa Yanga Fiston Mayele.