>

MGHANA HUYU AINGIA ANGA ZA YANGA

COLLINS Opare nyota wa Dodoma Jiji anatajwa kuwa kwenye hesabu za kusajiliwa na Yanga kwa ajili ya kuongeza makali kwenye safu ya ushambuliaji.

Raia huyo wa Ghana ni miongoni mwa washambuliaji wenye mchango mkubwa ndani ya Dodoma Jiji akiwa ametupia kambani mabao 9.

Kwenye mchezo uliopita dhidi ya Namungo wakiwa ugenini bao pekee la ushindi lilifungwa na Opare mwenye ushikaji mkubwa na Bernard Morrison nyota wa Yanga.

Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo dhidi ya Yanga uliochezwa Uwanja wa Azam Complex ubao uliposoma Yanga 4-2 Dodoma Jiji, Opare ni miongoni mwa nyota waliofunga.