>

VITA MPYA IMEIBUKA YANGA V SIMBA

WAKATI vita ya ubingwa ikiwa imefungwa kwa Yanga kufanikisha lengo la kutwaa ubingwa suala la kiatu cha ufungaji bora kwa sasa kina sura mpya.

Ni Fiston Mayele mshambuliaji wa Yanga huyu anaongoza kwenye orodha akiwa ametupia mabao 16 na pasi tatu za mabao.

Anayemfuatia ni Saido Ntibanzokiza wa Simba mwenye mabao 15 kibindoni na pasi 12 za mabao.

Nyota huyo kasi yake ilikuwa ya kusuasua kwenye mechi za nyuma kama alivyokwama kufunga dhidi ya Namungo lakini kwenye mchezo dhidi ya Polisi Tanzania alipachika mabao matano na bao moja likifungwa na Israel Mwenda.

Mchezo mmoja mkononi kwa timu zote hivyo mfungaji bora anasubiri dakika 90 zimeguke ndipo atatambulika kuwa yupi anasepa na tuzo hiyo.

Mchezo ujao Simba ni dhidi ya Coastal Union ya Tanga na Yanga ni dhidi ya Tanzania Prisons ya Mbeya,vita ya kiatu itakwenda kugota mwisho palepale baada ya dakika 90.

Ntibanzokiza anakuwa nyota wa kwanza kufunga mabao matano kwenye mchezo mmoja huku akiwa na hat trick mbili ndani ya ligi kama ambavyo anazo Bocco.

Mayele wa Yanga yeye ni nyota wa kwanza kufunga hat trick alifanya hivyo kwenye mchezo dhidi ya Singida Big Stars Uwanja wa Mkapa.