>

SIMBA YAICHAPA 6-1 POLISI TANZANIA, NTIBA, MWENDA WAWAKA

KIKOSI cha Simba kimeibuka na ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Polisi Tanzania kwenye mchezo wa mzunguko wa pili, Uwanja wa Azam Complex.

Mzawa Israel Mwenda amepachika bao moja kwenye mchezo wa leo dakika ya 65 akitumia majalo ya Shomari Kapombe.

Mabao matano kwa Simba yamefungwa na Saido Ntibanzokiza dakika ya 15,20, 26, 78 na dakika ya 89.

Anafikisha mabao 15 ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2022/23 akiwa ni namba mbili kwa utupiaji na namba moja ni Fiston Mayele mwenye mabao 16 kibindoni ni mali ya Yanga,

Bao la kufutia machozi kwa Polisi Tanzania ambayo haina uhakika wa kubaki ndani ya ligi limefungwa na Henck Mayala dakika ya 85 akimtunga Ally Salim