INJINIA Hersi Said, Rais wa Yanga amesema kuwa watandoka na ndege maalumu leo Juni 5 kuelekea Mbeya ikiwa imelipiwa na Serikali.
Yanga baada ya kufika fainali na kumaiza kwa ushindi dhidi ya USM Alger licha ya kushindwa kutwaa ubingwa walicheza mchezo wa ushindani katika kusaka nafasi ya kutwaa ubingwa lakini malengo hayakutimia.
Kutokana na hayo Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan aliwapa pongezi na kuwaalika Juni 5 kwenye hafla fupi Ikulu, Dar.
Injinia Hersi amesema:’Ndege yetu kuelekea Mbeya kwenye mchezo wa Ligi Kuu ilikuwa ni saa 1 usiku lakini Mheshimiwa Rais ametualika Dinner baada ya kutoa taarifa yetu kuwa Safari yetu ni saa moja, Mhe. Rais amelipa ndege maalum itakayoipeleka Yanga Mbeya.
“Ndege itaondoka Dar es Salaam saa 5 usiku, kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Mbeya City ambao ni muhimu kwetu kupata ushindi hivyo kwa hili tunamshukuru sana,”.
Yanga iligotea nafasi ya mshindi wa pili kwenye Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi na nahodha ni Bakari Mwamnyeto.