KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema kuwa wachezaji wake wana kazi kwenye mechi mbili zilizobaki kupata matokeo mazuri.
Yanga imetwaa ubingwa ikiwa na pointi 74 baada ya kucheza mechi 28 kwenye ligi na imepoteza mechi mbili pekee dhidi ya Ihefu na Simba.
Mechi mbili ambazo zimebaki ni dhidi ya Mbeya City inayotarajiwa kuchezwa juni 6 na ile dhidi ya Tanzania Prisons ambayo inatarajiwa kuchezwa Juni 9.
Nabi amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa kwa wachezaji wake kukamilisha msimu kwa kupata matokeo mazuri.
“Tuna kazi kubwa ya kufanya kwenye mechi zetu za ligi ambazo zimebaki tunaamini zitakuwa ngumu kutokana na timu ambazo tunakutana nazo kuhitaji ushindi pia.
“Kikubwa kila mmoja kutimiza majukumu yake kwa wakati, ninaamini kwamba tutafanya vizuri na kupata matokeo mazuri kwenye mechi zetu zijazo,” amesema Nabi.