BERNARD Morrison kiungo wa Yanga ameivuruga rekodi yake aliyoiweka akiwa ndani ya Simba kwa kuandika rekodi nyingine ndani ya Ligi Kuu Bara.
Rekodi zinaonyesha kuwa Morrison alipokuwa ndani ya Simba alipogotea kwenye dakika 699 alifunga bao moja na kutengeneza pasi mbili za mabao huku akiwa ndani ya Yanga akiwa amepukutusha dakika 692 katupia mabao matatu akiwa amecheza mechi 14 na kutengeneza pasi mbili za mabao.
Mabao yote ambaye amefunga katupia akiwa ndani ya 18 akitumia mguu wa kulia chini ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.
Bao la kwanza akiwa ndani ya Simba 2021/22 alipocheza mechi 12 Morrison alifunga dhidi ya Coastal Union mchezo uliochezwa Aprili 7,2022, Mkwakwani,Tanga akiwa ndani ya 18 dakika ya 39.
Pasi yake ya kwanza ndani ya Simba alitoa kwenye mchezo dhidi ya Ruvu Shooting dakika ya 17 akiwa nje ya 18 pasi yake ya pili alitoa kwenye mchezo dhidi ya Geita Gold ilikuwa Desemba Mosi dakika ya 55 akiwa nje ya 18.
Bao lake la kwanza kawatungua Coastal Union msimu huu akiwa na Yanga, Geita Gold kwa mkwaju wa penalti na Kamba ya tatu ilikuwa mchezo dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Azam Complex yote akitumia mguu wa kulia akiwa ndani ya 18.