BEKI WA KAZIKAZI AMEANZA KAZI SIMBA

BEKI wa kazi ngumu ndani ya kikosi cha Simba ambaye amekuwa nje ya uwanja kwa muda Mohamed Ouattara hatimaye ameanza mazoezi.

Nyota huyo hakuwa fiti baada ya kupata maumivu alipokuwa kwenye majukumu yake.

Alikuwa miongoni mwa nyota waliopata nafasi ya kucheza mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Katika mchezo huo zama za Kocha Mkuu Zoran Maki ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga 2-1 Simba na alikuwa shuhuda wa taji la kwanza likielekea Jangwani.

Simba inafanya maandalizi ya mechi mbili za Ligi Kuu Bara kukamilisha mzunguko wa pili ndani ya 2022/23.

Ni dhidi ya Polisi Tanzania unaotaraiiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex Juni 6,2023.

Ahmed Ally Meneja wa Idara ya Habari amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mechi zilizobaki kupata matokeo chanya.