WAARABU WAKOMAA A FISTON MAYELE

LICHA ya kupoteza mchezo wa kwanza wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika Jumapili Mei 28,2023 ubao wa Uwanja wa Mkapa uliposoma Yanga 1-2 USM Alger, jina la mshambuliaji Fiston Mayele lipo mikononi mwa Waarabu.

Juni 3,2023 mchezo wa fainali ya pili unatarajiwa kuchezwa na mshindi wa jumla atasepa na taji hilo kubwa Afrika.

Mayele mshambuliaji wa Yanga alifunga bao kwa upande wa Yanga dakika ya 82 linakuwa ni bao lake la saba kwenye mashinano hayo makubwa akiwa ni kinara wa utupiaji kiujumla.

Kocha Mkuu wa USM Alger, Abdulekh Banchikha alisema kuwa walicheza na wapinzani wazuri ambao walikuwa wanapambana kutafuta ushindi wakiongozwa na Mayele.

“Umeona ulikuwa ni mchezo mgumu kwa pande zote licha ya kwamba tulicheza mchezo mkubwa bado mshambuliaji wao Mayele, (Fiston) alifanya kazi nzuri na ni moja ya wachezaji wazuri.

“Niliwaambia wachezaji kuwa wanapaswa kucheza na timu kiujumla lakini wasimuache mshambuliaji wao ambaye alitufunga,bado kuna mchezo wa pili nyumbani bado kazi haijaisha kwa kuwa mpira una matokeo yake,” amesema Banchikha.