UONGOZI wa Azam FC Umesema hautakubali kufanya makosa ya kuwaachia mastaa muhimu waondoke bure baada ya mikataba yao kumalizika wakikumbuka ya msimu wa mwaka 2017.
Kwenye ligi Azam FC ipo nafasi ya tatu na ina pointi 53 vinara ni Yanga wenye pointi 74 na tayari wametangazwa kuwa mabingwa wa msimu wa 2022/23.
Azam katika msimu wa mwaka 2017 iliwaacha wachezaji muhimu ambao mikataba yao ilimalizika na kujiunga na Simba ambao nyota hao ni Shomary Kapombe,Aish Manula, Erasto Nyoni na John Bocco.
Kwa sasa inatajwa kuwa moja ya washambuliaji ndani ya kikosi cha Azam FC Prince Dube yupo kwenye hesabu za mabosi wa Simba wkihitaji kupata saini yake.
Mtendaji mkuu wa Azam FC,Popat alisema kuwa “Hatuwezi kurudia makosa ambayo tuliwahi kufanya huko nyuma,kwa sasa wachezaji wetu muhimu Hatuwezi kuruhusu waondoke bure,tutahakikisha kuwa tunawalinda kwaajili ya kutupa mafanikio huko mbeleni,” alisema kiongozi huyo.