SAKHO NA NYAVU NDANI YA LIGI KUU BARA

PAPE Sakho ndani ya Ligi Kuu Bara katupia mabao 9 msimu wa 2022/23 aligotea kwenye mabao hayo dhidi ya Ruvu Shooting, Uwanja wa Azam Complex.

Kinara wa utupiaji ni Fiston Mayele wa Yanga mwenye mabao 16 akiwa ametoa pasi mbili za mabao msimu wa 2022/23.

Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira amesema kuwa kiungo huyo anafanya kazi kubwa na ni miongoni mwa wachezaji wanaotimiza majukumu yao ndani ya uwanja.

Timu hiyo ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa imekusanya pointi 67 baada ya kucheza mechi 28.

“Wachezaji wetu wanapambana na kufanya kazi kubwa hilo linatupa nguvu ya kuwa kwenye mwendelezo mzuri wa mechi ambazo zimebaki.

“Bado kazi inaendelea na ukizungumzia wachezaji kila mmoja anafanya kazi yake kwa namna anavyopata nafasi ninafurahishwa na uwezo wa kila mmoja ikiwa ni Sakho, Clatous Chama, Henock Inonga,”..