MKIA wa pointi tatu kwa wababe Namungo na Simba umekuwa mkubwa kuliko na kuwafanya wagawane pointi mojamoja.
Simba walianza kupachika bao dakika ya 27 kupitia kwa Jean Baleke liliwaongezea hasira Namungo kusaka bao la kuweka usawa.
Ni Hassan Kabuda dakika ya 39 alimtungua Ally Salim akitumia makosa ya kipa huyo namba tatu kwenye kuokoa hatari.
Mpaka dakika 90 zinakamilika hakuna timu iliyopata nafasi ya kupachika bao na kuwafanya watoshane nguvu.
Simba inasepa na pointi nne za Namungo kwa kuwa mchezo wa kwanza iliibuka na ushindi wa bao 1-0 leo Mei 3 mambo yamekuwa magumu kwao.