SABABU MECHI S.B.S V YANGA/AZAM V SIMBA KUSOGEZWA MBELE

KWENYE mechi za Kombe la Azam Sports Federation hatua ya nusu fainali ratiba zimezogezwa mbele kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF).

Mchezo Kati ya Singida Big Stars dhidi ya Yanga ulitarajiwa kuchezwa Mei 7, Uwanja wa Liti utapangiwa tarehe nyingine.

Taarifa imeeleza kuwa Yanga inayoshiriki Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa hatua ya nusu fainali iliandika barua kuomba muda wa kufanya maandalizi mchezo dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini unaotarajiwa kuchezwa Mei 10, Uwanja wa Mkapa.

Pia mchezo wa Azam FC v Simba ulitarajiwa kuchezwa Mei 6 utachezwa Mei 7, Uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa sababu kubwa ya mchezo huo kupelekwa mbele ni kuzipa timu hizo mbili muda wa kutosha kuelekea maandalizi ya mchezo huo.