HUYU HAPA KOCHA MPYA AZAM FC

NI Youssouph Dabo ametambulishwa rasmi kuwa kocha mkuu wa Azam FC msimu ujao, 2023/24.

Dabo, raia wa Senegal, amesaini mkataba wa miaka mitatu kuwa ndani ya Azam FC.

Kwa sasa timu hiyo ipo chini ya Kali Ongala ambaye ni Kaimu Kocha Mkuu.

Kituo kinachofuata kwa Azam FC ni Jumamosi mchezo wa ASFC dhidi ya Simba, Nangwanda, Sijaona ikiwa ni hatua ya nusu fainali.