BAADA ya kutinga hatua ya nusu fainali Kombe la Shirikisho Afrika, Klabu ya Yanga inakuwa kwenye mashindano makubwa inayoshiriki.
Chini ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi raia wa Tunisia Aprili 30 iliandika rekodi yake mpya ya kutinga hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-0 Rivers United.
Mabao hayo yote Yanga ilishinda ikiwa ugenini na mfungaji alikuwa ni Fiston Mayele akitumia pasi za Bakari Mwamnyeto.
Katika mchezo wa robo fainali ya pili safu ya ulinzi ya Yanga iliimarisha ngome yake ikifanya kazi kwa ushirikiano kati ya Nondo, Dickson Job, Kibwana Shomari na Bacca ambapo Djigui hakutunguliwa.
Ni Kombe la Azam Sports Federation sasa wanashiriki wakiwa hatua ya nusu fainali ambapo watacheza na Singida Big Stars pamoja na Ligi Kuu Bara.
Mashindano yote mawili ya nyumbani Yanga ni bingwa mtetezi na kete yake ya tatu ni nusu fainali Kombe la Shirikisho Afrika.
Ni dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini Yanga inatarajiwa kuvaana nao kwenye mchezo wa nusu fainali mchezo unaotarajiwa kuchezwa Mei 10, Uwanja wa Mkapa.