BAADA ya kugotea hatua ya robo fainali msafara wa kikosi cha Simba umewasili salama Dar, leo Aprili 30,2023.
Kikosi cha Simba chini ya Kocha Mkuu, Roberto Oliveira kilikuwa na kazi ya kuwavua ubingwa mabingwa watetezi Wydad Casablanca ila ngoma ikawa nzito kwao.
Jumla ya penalti 4-3 zimewaondoa kwenye reli Simba baada ya matokeo ya jumla kuwa 1-1 ambapo kila timu ilishinda kwenye uwanja wa nyumbani.
Kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Simba ilishinda mchezo huo na kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mohamed V ni Wydad walishinda mchezo huo.
Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira amesema kuwa wachezaji walijituma na walikuwa wanahitaji kusonga mbele lakini haikuwa bahati kwao.
Kikosi hicho kina mechi za ushindani kwenye Kombe la Azam Sports Federation dhidi ya Azam FC na kwenye ligi dhidi ya Namungo.