MASTAA HAWA SIMBA WAPENYA KUWANIA TUZO

KIPA namba tatu wa Simba, Ally Salim ameingia kwenye mchakato wa kuwania tuzo ya mchezàji Bora wa mashabiki Kwa mwezi Aprili.

Hiyo ni tuzo maalumu inayotolewa ndani ya Simba kwa udhamini wa Emirate Aluminium Profile.

Ni mechi nne kakaa langoni Salim ambapo upepo unaoyesha kuwa anaweza kusepa nayo.

Ni Jean Baleke na Kibu Dennis hawa wanampa upinzani mkubwa mzawa huyo ambaye ametunguliwa bao moja kàtika mechi hizo nne.

Tayari kikosi kimeanza safari ya urejea Bongo kikitokea Morocco na kete yake inayofuata ni dhidi ya Azam FC mchezo wa hatua ya nusu fainali Kombe la Azam Sports Federation.